KWA: WATANZANIA WANAOISHI KUWAIT
YAH: KUOMBA PASIPOTI MPYA YA MFUMO WA KIELEKTRONIKI
Ubalozi unapenda kuwafahamisha kuwa, Ubalozi umeanza kufanya mchakato wa upatikanaji wa pasipoti mpya yenye mfumo wa Kielektroniki.
UTARATIBU WA KUOMBA:
Maombi haya ya kupata pasipoti mpya yanafanyika kwa njia ya mtandao (internet) hivyo Mwombaji atapaswa kuomba moja kwa moja kwenye mtandao kwa kupitia tovuti ya www.kw.tzembassy.go.tz au www.immigration.go.tz kisha utabonyeza e-service kisha utachagua 'Passport Application Form' kisha Mwombaji atajaza fomu na baadae ataprint fomu hiyo na kuja nayo katika Ofisi za Ubalozi kwa kuendelea na taratibu nyengine.
ANGALIZO
Mwombaji ahakikishe ana nyaraka zifuatazo kabla ya kujaza fomu:
(a) Cheti cha Kuzaliwa cha Mwombaji/ Barua ya Kiapo (Affidavit) kwa wasio na cheti cha kuzaliwa
(b) Cheti cha Kuzaliwa cha Mzazi mmoja wa Mwombaji/Barua ya Kiapo (Affidavit) kwa wasio na cheti cha kuzaliwa
(c) Picha 1
(d) Kitambulisho cha Taifa/Mpiga Kura (Kama unacho, si lazima)
(e) Nakala ya Pasipoti
(f) Nakala ya Residency Permit
(g) Nakala ya Kitambulisho cha Makazi (Civil ID)
NB: Kama utahitaji msaada wowote, wasiliana na Maafisa wa Ubalozi kwa maelekezo zaidi. Bw. Yussuf Abdalla, Mob: 50408564
Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu.
UBALOZI WA TANZANIA
KUWAIT
BY: UTAWALA