Mheshimiwa Mhandisi Aisha Salim Amour, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait, ashiriki katika Maonyesho ya Nchi za Afrika yaliyofanyika mwezi Desemba 2019. Kila mwaka Balozi za Nchi za Afrika zenye Uwakilishi nchini Kuwait kwa kushirikiana na Mfuko wa Fedha wa Kuwait (Kuwait Fund) huandaa maonyesho ya 'AFRICA DAY CELEBRATION' yenye lengo la kutangaza Nchi za Afrika kupitia Utalii, Biashara, Uwekezaji, Utamaduni na Sanaa. Ubalozi wa Tanzania nchini Kuwait ulishiriki maonyesho hayo yaliyofanyika mwezi Desemba, 2019.
Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait akiwa na Mabalozi wa nchi za Afrika zenye Uwakilishi nchini Kuwait kwenye sherehe za Maonyesho ya SIKU YA AFRIKA - KUWAIT
Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour, Balozi wa Tanzania nchini akiwa na Maafisa wa Ubalozi, Bi. Mtumwa S. Bakari pamoja na Bw. Yussuf J. Abdalla katika Banda la Maonyesho la Tanzania katika Sherehe za SIKU YA AFRIKA - KUWAIT