Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait, ametia saini Hati ya Makubaliano ya Mradi wa Umwagiliaji wa Bonde la Mto Luiche kati ya Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika hafla hiyo ya utiaji saini wa Hati hiyo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliwakilishwa na Mhe. Balozi, Mhandisi Aisha Salim Amour kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na kwa upande wa Kuwait Fund, makubaliano hayo yalitiwa saini na Mhe. Abdulwahab Ahmed Al-Bader, Mkurugenzi Mkuu, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mheshimiwa Dkt. Ahmed Nasser Al Mohammed Al Sabah ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait.