Tarehe 10 Machi, 2020, Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, atembelea ofisi za Mamlaka ya Kilimo na Uvuvi ya Kuwait na kufanya mazungumzo na Mtukufu Mohamed Al-Yousef Al-Sabah, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo.  

Mtukufu huyo alieleza utayari wa kushirikiana na Mamlaka za Tanzania katika sekta ya kilimo na uvuvi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika tafiti na teknolojia mbalimbali hasa katika mbegu, kilimo cha umwagiliaji na mbolea.

  • Tarehe 10 Machi, 2020, Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, akiangalia mashamba ya tafiti ya kilimo cha mbogamboga kwa kilimo cha kisasa greenhouse.