Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, atembelea Ofisi za Mamlaka ya Bandari ya Kuwait na kukutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Yousef Abdullah Sabah al-Nasser Al-Sabah, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari ya Kuwait.

Mazungumzo yao yalilenga ushirikiano kati ya Mamlaka ya Bandari ya Tanzania na Mamlaka ya Bandari ya Kuwait kwa maslahi ya nchi zote mbili.