Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, afanya mazungumzo na Mhe. Abdulwahab Ahmed Al-Bader, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) katika ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo. Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Kuwait Fund ambayo yapo kwa muda mrefu tokea mwaka 1975.
Balozi Mhandisi Aisha S. Amour afanya mazungumzo na Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait
